Showing posts with label MAGONJWA YA ZINAA. Show all posts
Showing posts with label MAGONJWA YA ZINAA. Show all posts

Friday, July 24, 2020

U.T.I

U.T.I : INA TIBIKA SASA KWAKUTUMIA DAWA ZA ASILI
UTi ni ugonjwa ambao unasumbua watu wengi; watoto, vijana na watu wazima.
UTI (Urinary Tract Infection); ni maambukizi kwenye njia ya mkojo. ambayo chanzo chake kikubwa kipo kwenye sehemu ya haja kubwa(anus)au kwenye utumbo mpana(large intestine)
kwanini imekua u.t.i?kabla ya kua u.t.i kulikua na vimelea ambavyo vinaishi katika eneo la haja kubwa ambavyo ni ulinzi wa eneo hilo,ila ukivihamisha kutoka eneo hilo nakupeleka eneo lingine haviwi ni ulinzi bali ni mashambulizi,
kwa kawaida mwanamke ameumbwa na centimetre 1-4 kutoka nje kwenda ndani kwenye njia yake ya haja ndogo,
ila tu milango yako ipo wazi sana na ni rahisi kupata maambukizi,

sasa wanawake wengi baada ya kujisaidia haja kubwa hujisafisha kutoka nyuma kwenda mbele na hapo ndipo wanapohamisha vile vimelea na vikifika njia ya mkojo vinakua ni mashambulizi na ndipo vinaitwa (urinary track infection)U.T.I.
na ukishapata hivo vibacteria kwanza vinaenda kudhoofisha kinga za uke(normal flores)ambao hao normal flores wenyewe hua wanaishi kwenye ute wa kike(lactic acid) hivyo inakua ni rahisi kupata mashambulizi ya magonjwa mbalimbali.
Ugonjwa huu hushambulia
(1) Figo (kidneys);
(2) Ureters; ambayo ni mirija inayounganisha figo na kibofu cha mkojo,
kibofu cha mkojo (bladder) na urethra; sehemu inayotoa mkojo toka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili.
AINA ZA U.T.I
A) lower U.T.I
Lower U.T.I ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na
kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, mgonjwa atasikia dalili
zifuatazo:-
1. Maumivu wakati wa kukojoa
2. Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo 
     kidogo tu
3. Damu katika mkojo
4. Mkojo wenye rangi ya chai
5. Mkojo wenye harufu kali
6. Maumivu ya kiuno kwa wanawake
7. Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume
B. Upper U.T.I
Upper U.T.I ni maambukizi ya ndani ya figo. Hii ni hatua mbaya sana
endapo bacteria wataanza kuingia kwenye mkondo wa damu kutoka
kwenye figo – SEPSIS. Sepsis huweza kusababisha msukumo wa
damu kuwa mdogo sana (Low Blood Pressure), mshituko au kifo.
Dalili za upper UTI ni:
1. Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo
2. Homa
3. Kusikia baridi
4. Kusikia kichefuchefu
5. Kutapika
Ukiipuuza U.T.I Unaweza kupata athali kubwa sana kama zifuatazo
1.Figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure)hii ni hatari 
    sana ,hutokana na bacteria kushambulia figo
2.Kupatwa magonjwa ya kibofu ,kama kibofu kuziba 
   ,kushindwa kukojoa ,hii hupelekea MTU kukojoa kwa mirija
3.Maumivu ya mgongo, kiuno na NYONGA
4.Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.nk.
5.Kuharibu homon(hormon inbalance)
6.Mimba kuharibika
7.Kishindwa kubeba mimba.
PIA TUNATIBU
U.t.I sugu inayojirudiarudia
Fangasi(miwasho mwilini)
Nguvu za kiume Kwa dozi 1 tu.
Uzazi
Utokwaji Wa Uchafu kama maziwa mtindi ukeni tena 
kwa dozi 1 tu.
Tezi dume
Sukari
Presha
Vidonda vya tumbo
Pumu
Vimbe mbalimbali
Maumivu makali wakati Wa hedhi/kupitiliza na 
kutokuona kabisa
Bawasili

Wasiliana nami Dr. Kamfirimbisi kwa namba za simu
+255655531702 ,+255623450753, 255766105099


Saturday, July 18, 2020

TETEKUWANGA


UFAHAMU UGONJWA WA TETEKUWANGA:
TETEKUWANGA NI NINI?
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi kwa jina la varicella zooster, ugonjwa huu hushambulia mfumo wa hewa wa upumuaji.
Baadae ugonjwa huu hushambulia maini, bandama kisha huenda kwenye ngozi, kwenye ngozi ugonjwa huu huleta upele mwingi mwilini.
Ugonjwa huu hushambulia watoto wenye umri wa miaka mitano mpaka kumi lakini huweza kushambulia umri wowote ule.
Ukishapata ugonjwa huu huwezi kuugua tena lakini ikitokea kinga yako ikashuka sababu ya ugonjwa kama ukimwi, kisukari au mlo mbovu ugonjwa huu hurudi kama mkanda wa jeshi.
Ugonjwa unaambukizwaje?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya hewa au kugusana na mgonjwa na baada ya siku 11 mpaka 20 baada ya kuambukizwa dalili za kwanza za ugonjwa huu hutokea.
DALILI ZA TETEKUWANGA NI ZIPI?
Mwanzoni kabisa huanza homa, kikohozi na mwili kuchoka baadae ngozi hujaa vipele vikubwa vinavyowasha ambavyo husambaa kwanzia usoni, mikononi, miguuni na tumboni
Jinsi ya kugundua ugonjwa:
vipimo vya maabara sio lazima kwani ugonjwa unaweza kugundulika kwa kuangalia vipele na kuvitambua kama picha inavyoonyesha.
MATIBABU:
mgonjwa huweza kupona bila dawa yeyote lakini kwa mgonjwa ambaye kinga yake imeshuka anaweza kupewa dawa ya kupunguza makali ya ugonjwa. Baada ya wiki moja mpaka mbili vipele huanza hukauka kabisa na kwa kutoa maji na kuacha makovu.
MADHARA YA KUUGUA UGONJWA HUU:
Ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo ya moyo,figo, ini, kifua, jointi za miguu na mikono, na matatizo ya mishipa ya fahamu.
Jinsi ya kuzuia ugonjwa huu:
Mgonjwa anatakiwa atengwe mbali na watu wengine huku nguo zake na mashuka yake yakifuliwa kwa makini sana kwa kutumia gloves ili kutoambukiza watu wengine.


Sunday, July 12, 2020

DUDUMIZI


Dudumizi ni ndege anaye patikana porini. Katika ukanda wa Pwani, ndege hawa wanapatikana kwa wingi sana katika mapori ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Kisarawe vijijini ( Hususani katika vijiji vya Mwaneromango, Nzenga na Msanga ) pamoja na wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Ndege hawa wana macho mekundu, mkia mrefu pamoja na kucha ndefu sana.
Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga na wanyama wadogo pia.
Dudumizi wengi wana mabawa yenye rangi ya kahawia nyekundu na kichwa cheusi. Lakini pia wapo Dudumizi wenye mkia wa rangi ya shaba, Dudumizi weusi,Dudumizi wenye koo lenye rangi nyeusi, Dudumizi wenye kichwa chenye rangi ya buluu, pamoja na Dudumizi wenye nyushi nyeupe.
MAAJABU YA DUDUMIZI.
Dudumizi ni ndege mwenye maajabu mengi sana, kwa muwa muda hauturuhusu, leo nitataja mawili tu.
AJABU LA KWANZA : Ana uwezo wa kujifungua kamba mwenyewe. Kwa mfano, ukienda kwenye kiota cha Dudumizi, halafu ukawafunga makinda wa Dudumizi kamba kisha ukafunga na kwenye mti. Kesho yake asubuhi unakuta ile kamba imejifungua yenyewe . Ukimnchukua Dudumizi ukampeleka nyumbani kwako, ukamuweka kwenye banda, halafu ukamfunga kamba akiwa bandani, ukafunga banda halafu kamba hiyo ukaenda kuifunga kwenye mti au kitu chochote kile, kesho yake unakuta Dudumizi amefungua hiyo kamba na kuondoka, hata kama kamba hiyo itakuwa kubwa na nzito kwa kiasi gani.
AJABU LA PILI : Kwa kawaida Dudumizi hutaga mayai kati ya mawili hadi matano. Dume la Dudumizi ambalo huwa dogo kwa umbo kuliko jike, ndio linalo hatamia mayai na kutunza makinda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
1.Kamba iliyo tumika kuwafunga Dudumizi na ikajifungua yenyewe, ikichanganya na ndumba za kichawi pmaoja na vizimba vyake, hutumika kuwafungua kichawi, watu walio katika vifungo mbalimbali vya kichawi kama vile vifungo katika biashara, vifungo katika mapenzi na ndoa, vifungo katika rizki , vifungo vya mizimu, nakadhalika.
2.Dudumizi hutumika, kutengeneza ndumba maalumu kwa wale wanawake wanao penda kuwa inamisha waume zao.

Friday, July 3, 2020

CHUMVI YA MAWE


1.KUMUOMBA M/MUNGU SANA
Kumuomba mwenyezi mungu sana kwa imani yako itasaidia sana kufanya nyumba yako kuwa na nuru na nuksi kuondoka

2.CHOMA CHUMVI YA MAWE.
Choma chumvi ya mawe nyumbani kwako na katika vyumba pia huondoa sana nuksi katika nyumba,vyumba na sehemu ya bishara. Ila hakikisha chumvi iwe imetokana na maji ya bahari

3.CHOMA UDI
Hii ni njia iliyotumika sana na watu wa dini. Udi huondoa nuksi na kuita malaika wema ndani ya nyumba



4.MAJI YA BAHARI
kupigia deki na maji ya bahari pia huondoa nuksi

5.KUEPUKA GIZA.
Usipende nyumba yako kuwa na giza pia epuka vitu vyeusi kutawala nyumba yako.

6.CRYSTALS
kama una uwezo nunua mawe ya madini au crystals na weka ktk kona ya nyumba yako. penda sana crystal za kijani,nyeupe na blue

7.KUKARIBISHA WAGENI HASA WATOTO
kukaribisha wageni kwa kuwapikia ama kuwanywesha itu halali husaidia kuondoa nuksi nyumbani kwako

8.KUWASHA MISHUMAA

penda kuchoma mishumaa mitatu mieupe miwili na orange mmoja. inaaminika mishumaa ni njia kubwa ya kujitibu na kuondoa nuksi. mishumaa mieupe huleta nuru na ulinzi pia orange huondoa uadui mahara flani.
njia hii ya mishumaa hutumika sana na wazungu,wachina,wahindi na watu weupe wengi sana
ni vizuri unapochoma basi kutia nia zako kisha kufanya dua/maombi kwa imani yako vile utakavyo.

Monday, June 29, 2020

MJAFARI

FAIDA YA MTI WA MJAFARI KATIKA TIBA :
Asalam alykumu nyote.Tufahamu kwamba mti huu una faida kubwa sana hususani katika masuala ya tiba.Mti huu una mambo makubwa sana kwani,hutibu matatizo ya chango,vidonda vya tumbo,UTI,gonolea na kaswende,kikohozi,meno,kifafa,kisukari,malaria,taifodi,T.B,huzuia kuharisha na kutapika.Mjafari kuanzia majani yake ni mvuto wa ajabu,mbegu zake na mizizi ni tiba kubwa kwa wenye matatizo ya mchango ukipata unga wake utatumia kijiko kimoja cha cha kula x3.Mjafari mujarabu katika kusafisha nyota na kukufanya uwe maarufu ama ukihitaji kutoa nuksi,majini wachafu na vifungo tumia mjafari.Nitaelezea namna ya kutoa nuksi,majini wabaya,vifungo,na kusafisha nyota kwa kutumia mjafari jiunge katika group langu la Dr.kamfirimbisi kupitia whatsapp 0623 450753  tiba ya kweli ufumbuzi wa matatizo ya uchawi,vifungo na nuksi upate mengi zaidi.Kwa tiba mbalimbali tuwasiliane
Endapo unatatizo hili basi wasiliana na Dr. Kamfirimbisi kwa kutumia Simu:+255655531702/+255623450753/+255766105099 au kwa link ya whatsapp hapa chini



Bonyeza Link DR.KAMFIRIMBISI

Wednesday, June 24, 2020

MTU ALIYE PALIWA

IFAHAMU HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEPALIWA
kupaliwa ni nini?
hii ni hali ya kukabwa na kitu kwenye koo ya hewa, inaweza kua chakula kitu chochote ambacho mtu alikua anakichezea mdomoni na hatimaye kikaenda kukwama kwenye koo la hewa.
Ripoti ya shirika la afya duniani lilionyesha kwamba zaidi ya watu 162000 walifariki mwaka 2015 sababu ya kupaliwa na kukosa msaada wa haraka, idadi hiyo imetajwa kuongezeka muda unavyozidi kwenda lakini pia kupaliwa kunaweza kua hatari zaidi kwa watoto wadogo kwani anaweza kuweka kitu mdomoni na watu wakashindwa kujua kilichotokea.
mara nyingi watu hupaliwa na chakula, hela ya chuma, karanga, maharage,pini,kucha na kadhalika...         

                                         
Dalili za kupaliwa ni zipi?
mtu akipaliwa hua na dalili zifuatazo

kushindwa kuongea
kushindwa kupumua kawaida
kushindwa kukohoa
lips za mdomo kubadilika na kua blue sababu ya kukosa hewa
kupoteza fahamu.





Utamsaidia vipi mtu aliyepaliwa?
mtu akipaliwa kama nilivyotaja hapo juu hushindwa kuongea, anaweza kuja kwako mbio bila kusema chochote akawa anakonyesha kwa vitendo tu lakini pia unaweza kua uliona wakati anapaliwa hivyo fanya vifuatavyo..

mpige ngumi au makofi matano mgongoni kwa nguvu lakini 
usitumie nguvu sana hasa kama ni mtoto, ukiona bado kitu 
hakijatoka simama nyuma yake kisha weka mikono yako 
kwenye tumbo la mgonjwa karibu na kifua kama picha 
inavyoonyesha hapo juu lisha vuta kwa ndani na kuachia 
mara tano kitaalamu kama heimlich manouver, lakini hii ya 
kuweka mikono tumboni mtoto awe na zaidi ya mwaka 
mmoja.
ukiona kitu kilichompalia kimetoka na mgonjwa hapumui 
mlaze chini kisha kandamiza kifua na kuachia kitaalamu 
kama cardio pulmonary resuscitation baada ya hapo 
mgonjwa apelekwe hospitali kuangalia kama kuna madhara 
yeyote ameyapata.



mwisho; huduma hiyo ya kumsaidia mgonjwa inatakiwa ifanyike haraka baada ya mgonjwa kukabwa kwani kukosa kwa hewa ndani ya dakika tano huweza kuleta kifo, lakini pia ukipata elimu hii wafundishe jamaa zako na ndugu zako kwani ukipaliwa wewe hutaweza kujisaidia.


Saturday, June 20, 2020

KISUKARI

Ni Zipi Dalili Za Kisukari:

 Kisukari ni ugonjwa ambao humsababishia mtu kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu na kushindwa kuitumia sukari hiyo ipasavyo ili kumpa nguvu na hivyo sukari hiyo kutoka nje ya mwili wa mgonjwa kupitia njia ya mkojo. Ugonjwa huu pia huitwa Diabetes Mellitus, maneno yanayotokana na kigiriki na kilatini. Diabetes linatokana na kigiriki likimaanisha kijibomba kinachonyonya maji na mellitus linatokana na neno la kilatini “Mel” lenye maana ya asali, hivyo diabetes mellitus ni “kunyonya maji yenye utamu kama asali” baada ya madaktari wa enzi hizo kugundua kuwa mkojo na damu ya mgonjwa wa kisukari vilikuwa na glucose kwa wingi sana.
Wachina wa zamani nao waligundua kuwa mchwa walijaa kwa kwingi kwenye eneo la mkojo wa mtu mwenye kisukari kutokana na mkojo huo kuwa mtamu na wakatoa neno “Sweet Urine Disease” -Ugonjwa wa kutoa mkojo mtamu.
Insulin Na Kongosho:
Insulin ni homoni inayotoa ishara kwa seli za mwili ili ziweze kuchukua glucose kotoka kwenye damu na kuitumia katika kuupa mwili nguvu na kuujenga. Kama kiwango cha insulin mwilini ni kidogo au hakuna insulin kabisa katika mwili, glucose haitachukuliwa na seli za mwili hivyo kusababisha mwili kuyeyusha mafuta yaliyomo mwilini ili upate nguvu.
Insulin karibu za wanyama wote hufanana, tofauti ni katika nguvu ya ufanyaji wake wa kazi. Kwa mfano, insulin ya nguruwe “Porcine insulin”, inafanana sana na insulin ya binadamu, hii ikiwa na maana kuwa binadamu anaweza kutumia insulin ya wanyama. Lakini kwa bahati nzuri, insulin inaweza kutengenezwa kwenye maabara.
Kongosho ni sehemu ya viungo vilivyo katika mfumo wa uyeyushaji (mmeng’enyo) wa chakula na kinapatikana sehemu ambapo mbavu hukutana kwa chini. Kongosho lina umbo la jani na lina urefu upatao kama nchi sita. Kongosho ina kazi ya kutengenza insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula.
Dalili Za Kisukari Ni Zipi:
Baada ya kujikumbusha hayo, sasa tutazame mambo ambayo yakikutokea ujue kwamba ni dalili za kuwa na ugonjwa huu wa kisukari. Watu wengi wanakuwa na ugonjwa huu bila kujijua kwa sababu dalili za awali za ugonjwa huu hazimsababishii mtu kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida, lakini ni vizuri kuugundua ugonjwa huu katika hatua zake za awali ili kuepukana na madhara makubwa yanayoweza kutokea baadaye. Tutaorodhesha hapa dalili zinazojionyesha mara nyingi zaidi:
Kukojoa mara kwa mara: Jee, umekuwa na tabia ya kwenda kupata haja ndogo mara kwa mara? Kama jibu ni ndiyo, basi figo zako sasa haziwezi kuirudisha glucose kwenye mfumo wa damu na badala yake zinachukua maji kutoka kwenye damu na kusababisha kibofu kijae mara kwa mara.
Kiu Isiyoisha: Kama unakojoa mara kwa mara, utapata kiu isoisha kwa sababu mwili unahitaji kurudisha maji uliyopoteza kwenye mkojo.
Njaa Kali: Kama isulin yako haifanyi kazi au kama huna insulin, mwili wako unakosa glucose ya kuupa nguvu. Katika kutafuta njia nyingine ya kupata nguvu, mwili utakuwa na njaa ili uupatie chakula.
Kuongezeka kwa uzito (unene): Hii inatokana na dalili ya kusikia njaa kali.
Kupungua uzito kusiko kawaida: Hili huwatokea zaidi wagonjwa wa Type 1 Diabetes kwa sababu kwa kukosa insulin na seli kukosa chanzo cha kupata nguvu, mwili huanza kuvunjavunja misuli na kuyeyusha mafuta ya mwili ili upate nguvu hiyo, hali inayochangiwa zaidi na tabia ya kisukari cha aina hiyo kujitokeza kwa ghafla.
Uchovu wa mwili: Mwili unapokosa glucose ya kuzipa seli nguvu, uchovu hutokea.
Kutoona vizuri: Ugonjwa huu husababisha mtu kushindwakuviona vitu vizuri. Tatizo hili hutibika lakini mara nyingine halihuweza kuwa mbaya kiasi cha kuwa na tatizo la kudumu au kupata upofu.
Vidonda kutopona vizuri au haraka: Unapokuwa na sukari nyingi katika damu, uwezo wa mwili kuponya vidonda hupungua.
Magonjwa ya ngozi: Mwili wenye sukari nyingi ndani ya damu huwa na uwezo mdogo sana wa kujiponya kutokana na maambukizi ya wadudu. Wanawake wenye kisukari huwa na maambukizi zaidi na hupata shida kubwa ya kuponya maambukizi ya sehemu nyeti za miili yao.
Kuwashwa kwa ngozi: Kuwashwa kwa ngozi mara nyingine ni dalili ya kuwa na kisukari.
Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba: Fizi nyekundu na/au zilizovimba huweza kuwa ni dalili ya kuwa na ugonjwa wa kisukari, na mara nyingine meno hulegea.
Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa: Hili ni tatizo hasa la wanaume wenye umri unaozidi miaka 50, ambapo mara nyingi watakosa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kikamilifu au uwezo wao wa kufanya tendo hilo kufa kabisa (Erectile Dysfunction).
Ganzi mikononi au miguuni: Uzidifu wa sukari mwilini huweza kuharibu neva au mishipa midogo ya damu inayolisha neva, hivyo kusababisha hali ya ganzi mikononi au miguuni.
Madhara Ya Kisukari:
Kama ugonjwa wa kisukari hautadhibitiwa ipasavyo, madhara makubwa huweza kutokea. Baadhi ya madhara ambayo yamehusishwa na ugonjwa huu ni kama ifuatavyo:
Matatizo ya macho-glaucoma, cataracts na mengineyo.
Matatizo ya miguu-vidonda na gangrene ambavyo mara nyingine husababisha miguu ikatwe.
Matatizo ya moyo-pamoja na upungufu wa damu inayoelekea kwenye misuli ya moyo.
Hypertension-ambayo huweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi, matatizo ya macho, magonjwa ya moyo na kiharusi.
Matatizo ya kusikia-kisukari husababisho tatizo la kushindwa kusikia vizuri.
Gastroparesis-misuli ya tumbo kushindwa kufanya kazi yake vizuri.
Kiharusi (Stroke)-endapo blood pressure, cholesterol na sukari havitadhibitiwa, uwezekano wa kupatwa na kiharusi huwa ni mkubwa sana.
Ugumba-kisukari humfanya mgonjwa ashindwe kufanya tendo la ndoa


Contact Form

Name

Email *

Message *