Ushauri kwa wenyetatizo la hernia
Ngiri (Hernia) ni uvimbe
(eneo lililotuna) kutokana na viungo vya ndani ya mwili kusukuma kuta za misuli
inayozunguka au kushikilia viungo hivyo. Hernia hutokea wakati kuna udhaifu au
kuna tundu kwenye kuta za misuli inayoshikilia na kuviweka viungo vya tumbo
kwenye sehemu yake (peritoneum). Udhaifu huo unaweza kuviruhusu viungo vya
ndani kusukuma na kupenyeza, na kujenga eneo lililotuna. Unaweza kuwa na hernia
ikiwa unaweza kuhisi namna ya eneo laini lililotuna kwenye maeneo ya tumbo au
kinena au kwenye kovu ambalo lilitokana na upasuaji. Eneo hili lililotuna
linaweza likapotea ukiminya sehemu hiyo au ukijilaza. Unaweza kupata maumivu
kwenye eneo hilo hasa ukikohoa, ukiinama au ikinyanyua kitu kizito.
Hernia ni tatizo
linalowasumbua watu wengi katika nchi nyingi duniani. Hernia mara nyingi
hutokea kwenye maeneo ya tumbo, lakini huweza pia kutokea kwenye sehemu ya juu
ya mapaja, kwenye kitovu, na kwenye maeneo ya kinena. Hernia haihatarishi
maisha mara moja, lakini haiwezi kuondoka yenyewe na inaweza kuhitaji kufanyika
kwa upasuaji.
Hernia mara nyingi hupewa
majina kutokana na sehemu ya mwili inapojitokeza, ingawa mara nyingine majina
huweza kutolewa kutokana na sababu nyingine za kuitambulisha. Kila hernia
hutibiwa tofauti na nyingine kutokana na sehemu iliyopo na sababu nyingine za
kitaalamu. Kuwa na elimu ya kutosha ya kila aina ya hernia itakusaidia kujua
namna ya kutoa maamuzi sahihi ya tiba yake.
Aina Za Hernia
1. Inguinal (groin hernia)
Inguinal hernias au groin
hernias hutokea pale utumbo au mafuta yanaposukuma na kupenya kwenye misuli ya
eneo la kinena. Hii ndiyo aina ya hernia inayowasumbua watu wengi zaidi.
Inguinal hernia inaweza kuonekana kwa wanaume na wanawake lakini huwapata zaidi
wanaume kwa sababu tayari wana kijitundu kidogo kwenye misuli ya kinena kwa
ajili ya kupitisha arteri, veni na mrija wa mbegu vinavyoelekea kwenye
korodani. Asilimia 97 ya aina hii ya hernia huonekana kwa wanaume.
Hernia inaweza kuwa juu ya
misuli ya tumbo (direct inguinal hernia) au inaweza ikafuata njia ya mrija wa
shahawa pale unapoacha eneo la tumbo na kuelekea kwenye korodani (indirect
inguinal hernia). Inguianal hernia huanza kama uvimbe mdogo ambao huongezeka na
muda. Uvimbe unaoonekana ni utumbo au mafuta yanayosukuma misuli.
Uvimbe huweza kupotea kwa
kulala na kurudi mwili ukianza shughuli. Uvimbe huu ukiwa mkubwa sana, huenea
kutoka kwenye kinena hadi kwenye korodani zenyewe. Hernia ikiwa kubwa sana
huleta matatizo kuiondoa.
2. Umbilical (belly button hernia)
Belly button hernia au
umbilical hernia kama inavyoitwa mara nyingine, ni pale utumbo au mafuta
yanapopenya kupitia sehemu dhaifu ya misuli iliyopo katikati ya tumbo chini ya
kitovu. Sehemu hii ndiyo inayopata udhaifu mara nyingi kwa sababu ndiyo sehemu
inayopata minyumbuko zaidi wakati tukifanya shughuli yo yote ya mwili.
Umbilical hernia inaweza
kuwa moja kwa moja chini ya kitovu, lakini wakati mwingine inaweza kuwa juu
kidogo au chini kidogo ya kitovu. Inaweza kuonekana kama kijikokoto kidogo
chini ya ngozi, au ikikua inaweza kuonekana kama kijimpira cha gofu au hata
kufikia kimpira cha tenisi kama kikiachwa bila tiba.
Kwa watoto wa kufikia hadi
miaka 5, hernia hii kwa kawaida huondoka yenyewe. lakini kwa watu wazima hernia
hii haipungui na huwa inazidi kuwa kubwa kila wakati. Wanawake kwa kawaida
hupata umbilical hernia wakati wa ujauzito, na hupotea yenyewe baada ya
kujifungua. Kwa baadhi ya wanawake, kijishimo hiki katika musuli hubakia baada
ya kujifungua. Inashauriwa kuwa wanawake wasubiri kwa miezi 3-6 kuona kama
hernia hii itafunga yenyewe.
Kama ilivyo kwa hernia
nyingine, dalili za kawaida ni maumivu kwenye kitovu. Kutokana na mafuta au
misuli kupita kwenye hernia hii, uvimbe utaonekana chini ya ngozi kwenye eneo
hilo. Baada ya muda, kama hernia itakuwa kubwa sana, utumbo unaweza kunaswa
kwenye hernia hiyo na kuleta madhara kwenye utumbo, vikiambatana na
kichefuchefu, kutapika, na kufunga choo.
Kwa sababu hakuna hernia
inayopona yenyewe, upasuaji unahitajika. Njia inayopendekezwa hapa ni open
surgery kwa sababu tundu ni dogo.
3. Femoral (below the groin)
4. Epigastric (just below the breast bone)
5. Ventral (above the umbilicus)
6. Incisional (through a prior surgery site)
7. Sports
Namna nyingine za kuelezea
Hernia:
1. Recurrent (after a
prior hernia repair)
2. Unilateral (one side of the body)
3. Bilateral (both sides of the body)
Sababu Za Hernia
Ukiondoa hernia
inayotokana na upasuaji wa awali, mara nyingi hakuna sababu inayoeleweka ya
kusababisha hernia. Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata hernia ni wenye
umri mkubwa, na wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake.
Hernia inaweza kujitokeza
mtoto anapozaliwa au kwa watoto waliozaliwa na dosari kwenye kuta za matumbo
yao.
Shughuli au madawa
yanayosababisha mgandamizo kwenye kuta za tumbo vinaweza kusababisha hernia.
Vitu hivi ni pamoja na:-Kujikamua kwa nguvu wakati wa haja kubwa, kutokana
na choo kuwa kigumu,Kikozi cha mara kwa mara,Kuwa na tatizo la cystic
fibrosis,Kuvimba kwa tezi dume,Unene wa kupindukia,Kukojoa kwa
shida,Kunyanyua vitu vizito,Maji tumboni,Lishe duni uvutaji wa tumbaku,Korodani
zisizoshuka,Uchovu wa mwili
Dalili Za Hernia:-Mara nyingi, hernia ni uvimbe
unaoonekana usio na mauvimu na usiohitaji tiba ya haraka. Lakini wakati
mwingine, inaweza kukukosesha raha na kuwa na maumivu, dalili zikiongezeka
wakati umesimama au wakati unanyanyua vitu vizito. Watu wengi huona uvimbe
ukizidi na hatimaye humwona daktari.
Kuna wakati ambapo hernia
inahitaji huduma ya haraka ya upasuaji, kwa mfano, pale sehemu ya utumbo
inapokuwa imezibwa na hernia ya tumbo (inguinal hernia).
Hatua za haraka za
uchunguzi zinatakiwa zichukuliwe wakati inguinal hernia inapoanza kuonyeza
dalili kali za:
. Maumivu
. Kusikia kichefuchefu
. Kutapika
Uvimbe wa hernia yenye
dalili hizi mara nyingi ni mgumu na huleta maumivu na hauwezi kusukumwa urudi
ndai ya tumbo.
Hiatal hernia inaweza
kuleta dalili za acid refluc kama kiungulia, kinachotokana na tindikali za
tumboni kupanda kwenye koromeo.