Kisukari ni ugonjwa ambao humsababishia mtu kuwa
na kiwango kikubwa cha sukari katika damu na kushindwa kuitumia sukari hiyo
ipasavyo ili kumpa nguvu na hivyo sukari hiyo kutoka nje ya mwili wa mgonjwa
kupitia njia ya mkojo. Ugonjwa huu pia huitwa Diabetes Mellitus, maneno
yanayotokana na kigiriki na kilatini. Diabetes linatokana na kigiriki
likimaanisha kijibomba kinachonyonya maji na mellitus linatokana na neno la
kilatini “Mel” lenye maana ya asali, hivyo diabetes mellitus ni “kunyonya maji
yenye utamu kama asali” baada ya madaktari wa enzi hizo kugundua kuwa mkojo na
damu ya mgonjwa wa kisukari vilikuwa na glucose kwa wingi sana.
Wachina
wa zamani nao waligundua kuwa mchwa walijaa kwa kwingi kwenye eneo la mkojo wa
mtu mwenye kisukari kutokana na mkojo huo kuwa mtamu na wakatoa neno “Sweet
Urine Disease” -Ugonjwa wa kutoa mkojo mtamu.
Insulin Na Kongosho:
Insulin
ni homoni inayotoa ishara kwa seli za mwili ili ziweze kuchukua glucose kotoka
kwenye damu na kuitumia katika kuupa mwili nguvu na kuujenga. Kama kiwango cha
insulin mwilini ni kidogo au hakuna insulin kabisa katika mwili, glucose
haitachukuliwa na seli za mwili hivyo kusababisha mwili kuyeyusha mafuta
yaliyomo mwilini ili upate nguvu.
Insulin
karibu za wanyama wote hufanana, tofauti ni katika nguvu ya ufanyaji wake wa
kazi. Kwa mfano, insulin ya nguruwe “Porcine insulin”, inafanana sana na
insulin ya binadamu, hii ikiwa na maana kuwa binadamu anaweza kutumia insulin
ya wanyama. Lakini kwa bahati nzuri, insulin inaweza kutengenezwa kwenye
maabara.
Kongosho
ni sehemu ya viungo vilivyo katika mfumo wa uyeyushaji (mmeng’enyo) wa chakula
na kinapatikana sehemu ambapo mbavu hukutana kwa chini. Kongosho lina umbo la
jani na lina urefu upatao kama nchi sita. Kongosho ina kazi ya kutengenza
insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula.
Dalili Za Kisukari Ni Zipi:
Baada
ya kujikumbusha hayo, sasa tutazame mambo ambayo yakikutokea ujue kwamba ni
dalili za kuwa na ugonjwa huu wa kisukari. Watu wengi wanakuwa na ugonjwa huu
bila kujijua kwa sababu dalili za awali za ugonjwa huu hazimsababishii mtu
kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida, lakini ni vizuri kuugundua
ugonjwa huu katika hatua zake za awali ili kuepukana na madhara makubwa
yanayoweza kutokea baadaye. Tutaorodhesha hapa dalili zinazojionyesha mara
nyingi zaidi:
Kukojoa
mara kwa mara: Jee, umekuwa na tabia ya kwenda kupata haja ndogo mara
kwa mara? Kama jibu ni ndiyo, basi figo zako sasa haziwezi kuirudisha glucose
kwenye mfumo wa damu na badala yake zinachukua maji kutoka kwenye damu na
kusababisha kibofu kijae mara kwa mara.
Kiu
Isiyoisha: Kama unakojoa mara kwa mara, utapata kiu isoisha kwa
sababu mwili unahitaji kurudisha maji uliyopoteza kwenye mkojo.
Njaa
Kali: Kama isulin yako haifanyi kazi au kama huna insulin,
mwili wako unakosa glucose ya kuupa nguvu. Katika kutafuta njia nyingine ya
kupata nguvu, mwili utakuwa na njaa ili uupatie chakula.
Kuongezeka
kwa uzito (unene): Hii inatokana na dalili ya kusikia
njaa kali.
Kupungua
uzito kusiko kawaida: Hili huwatokea zaidi wagonjwa
wa Type 1 Diabetes kwa sababu kwa kukosa insulin na seli kukosa
chanzo cha kupata nguvu, mwili huanza kuvunjavunja misuli na kuyeyusha mafuta
ya mwili ili upate nguvu hiyo, hali inayochangiwa zaidi na tabia ya kisukari
cha aina hiyo kujitokeza kwa ghafla.
Uchovu
wa mwili: Mwili unapokosa glucose ya kuzipa seli nguvu, uchovu
hutokea.
Kutoona vizuri: Ugonjwa
huu husababisha mtu kushindwakuviona vitu vizuri. Tatizo hili hutibika lakini
mara nyingine halihuweza kuwa mbaya kiasi cha kuwa na tatizo la kudumu au
kupata upofu.
Vidonda kutopona vizuri au haraka: Unapokuwa
na sukari nyingi katika damu, uwezo wa mwili kuponya vidonda hupungua.
Magonjwa ya ngozi: Mwili
wenye sukari nyingi ndani ya damu huwa na uwezo mdogo sana wa kujiponya
kutokana na maambukizi ya wadudu. Wanawake wenye kisukari huwa na maambukizi
zaidi na hupata shida kubwa ya kuponya maambukizi ya sehemu nyeti za miili yao.
Kuwashwa kwa ngozi: Kuwashwa
kwa ngozi mara nyingine ni dalili ya kuwa na kisukari.
Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba: Fizi
nyekundu na/au zilizovimba huweza kuwa ni dalili ya kuwa na ugonjwa wa
kisukari, na mara nyingine meno hulegea.
Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la
ndoa: Hili ni tatizo hasa la wanaume wenye umri
unaozidi miaka 50, ambapo mara nyingi watakosa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa
kikamilifu au uwezo wao wa kufanya tendo hilo kufa kabisa (Erectile
Dysfunction).
Ganzi mikononi au miguuni: Uzidifu
wa sukari mwilini huweza kuharibu neva au mishipa midogo ya damu inayolisha neva,
hivyo kusababisha hali ya ganzi mikononi au miguuni.
Madhara Ya Kisukari:
Kama ugonjwa wa kisukari
hautadhibitiwa ipasavyo, madhara makubwa huweza kutokea. Baadhi ya madhara
ambayo yamehusishwa na ugonjwa huu ni kama ifuatavyo:
Matatizo ya macho-glaucoma,
cataracts na mengineyo.
Matatizo ya miguu-vidonda na
gangrene ambavyo mara nyingine husababisha miguu ikatwe.
Matatizo ya moyo-pamoja na
upungufu wa damu inayoelekea kwenye misuli ya moyo.
Hypertension-ambayo huweza
kusababisha figo kushindwa kufanya kazi, matatizo ya macho, magonjwa ya moyo
na kiharusi.
Matatizo ya kusikia-kisukari
husababisho tatizo la kushindwa kusikia vizuri.
Gastroparesis-misuli ya tumbo
kushindwa kufanya kazi yake vizuri.
Kiharusi (Stroke)-endapo
blood pressure, cholesterol na sukari havitadhibitiwa, uwezekano wa kupatwa na
kiharusi huwa ni mkubwa sana.
Ugumba-kisukari humfanya
mgonjwa ashindwe kufanya tendo la ndoa