Sunday, July 12, 2020

DUDUMIZI


Dudumizi ni ndege anaye patikana porini. Katika ukanda wa Pwani, ndege hawa wanapatikana kwa wingi sana katika mapori ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Kisarawe vijijini ( Hususani katika vijiji vya Mwaneromango, Nzenga na Msanga ) pamoja na wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Ndege hawa wana macho mekundu, mkia mrefu pamoja na kucha ndefu sana.
Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga na wanyama wadogo pia.
Dudumizi wengi wana mabawa yenye rangi ya kahawia nyekundu na kichwa cheusi. Lakini pia wapo Dudumizi wenye mkia wa rangi ya shaba, Dudumizi weusi,Dudumizi wenye koo lenye rangi nyeusi, Dudumizi wenye kichwa chenye rangi ya buluu, pamoja na Dudumizi wenye nyushi nyeupe.
MAAJABU YA DUDUMIZI.
Dudumizi ni ndege mwenye maajabu mengi sana, kwa muwa muda hauturuhusu, leo nitataja mawili tu.
AJABU LA KWANZA : Ana uwezo wa kujifungua kamba mwenyewe. Kwa mfano, ukienda kwenye kiota cha Dudumizi, halafu ukawafunga makinda wa Dudumizi kamba kisha ukafunga na kwenye mti. Kesho yake asubuhi unakuta ile kamba imejifungua yenyewe . Ukimnchukua Dudumizi ukampeleka nyumbani kwako, ukamuweka kwenye banda, halafu ukamfunga kamba akiwa bandani, ukafunga banda halafu kamba hiyo ukaenda kuifunga kwenye mti au kitu chochote kile, kesho yake unakuta Dudumizi amefungua hiyo kamba na kuondoka, hata kama kamba hiyo itakuwa kubwa na nzito kwa kiasi gani.
AJABU LA PILI : Kwa kawaida Dudumizi hutaga mayai kati ya mawili hadi matano. Dume la Dudumizi ambalo huwa dogo kwa umbo kuliko jike, ndio linalo hatamia mayai na kutunza makinda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
1.Kamba iliyo tumika kuwafunga Dudumizi na ikajifungua yenyewe, ikichanganya na ndumba za kichawi pmaoja na vizimba vyake, hutumika kuwafungua kichawi, watu walio katika vifungo mbalimbali vya kichawi kama vile vifungo katika biashara, vifungo katika mapenzi na ndoa, vifungo katika rizki , vifungo vya mizimu, nakadhalika.
2.Dudumizi hutumika, kutengeneza ndumba maalumu kwa wale wanawake wanao penda kuwa inamisha waume zao.

Contact Form

Name

Email *

Message *