Monday, June 8, 2020

KOMAMANGA

FAIDA YA KOMAMANGA:(POMEGRANATE)
Mkomamanga ni mmea ambao asili yake ni katika nchi za mashariki ya kati.
Mkomamanga una dawa mbali mbali kama vile Tannis (punicalin na punicalagin), flavonoids, alkaloids, steroids, triterpenes na polyphenols.
Dawa hizi hupatikana katika magome, mbegu, majani, maganda ya matunda, juisi ya matunda yake na katika maua yake.
Tunda la komamanga pia lina vitamin C na E kwa wingi pamoja na madini ya potassium na copper.
Dawa zinazopatikana katika maganda na majani ya mkomamanga husaidia katika hali ya tumbo kujaa gesi na tindikali (acid) tumboni. Mkomamanga pia husaidia katika matibabu ya kuhara damu na kutibu maambukizo katika kibofu cha mkojo.
Lojo ya mbegu za matunda ya komamanga ikichanganywa na maziwa, husaidia katika tiba ya kuondosha mawe katika figo.
Fukuto ya mkomamanga husaidia katika tiba ya minyoo aina ya tegu (tapeworms) lakini pia husaidia katika matibabu ya uvimbe wa wengu (spleen) pamoja na kutibu vidonda vya tumbo.
  • Komamanga husaidia katika jitihada za kupambana na unene wa kupindukia (obesity)
  • Husaidia katika matibabu ya tatizo la ini pale linapoelemewa (liver congestion)
  • Dawa ndani ya komamanga licha ya kuwa na uwezo wa kudhibiti aina mbali mbali za bakteri wanaosababisha magonjwa mwilini, pia zina uwezo wa kutibu magonjwa ya muda mrefu kama vile saratani ya tezi ya prostate ya wanaume, saratani mbali mbali, kisukari, baridi yabisi na uvimbe wa maungio (gout)
  • Husaidia mwili kuondosha sumu na uchafu utokanao na kemikali na mabaki ya vyakula mwilini kama vile asidi ya uriki (uric acid). Sumu hizi ni chanzo kikuu cha magonjwa mengi ya kusendeka (muda mrefu)
  • Huweza kuzuia maendeleo ya saratani ya mapafu.
  • Hupambana na saratani ya matiti
  • Hupunguza ukuaji wa saratani ya kibofu
  • Inaweza kuzuia na kupunguza kasi ya ugonjwa wa Alzheimer
  • Inapunguza kolesterol
  • Hushusha shinikizo la damu na kufanya mzunguko wa damu kuwa vizuri.
  • Hulinda meno

Dawa lishe hii hutumiwa kwa kunywa fukuto inayotokana na sehemu za mmea kiasi cha gramu 3 hadi 9 kwa siku inatosha kwa ajili ya tiba ya magonjwa mbali mbali. Kwa ajili ya minyoo ya tegu magome au mizizi ya mkomamanga kiasi cha gramu 50 huchemshwa katika lita 1 ya maji ili kupata fukuto.
Juisi ya matunda yake pia inaweza kutumiwa kiasi cha bilauri 1 kila siku ili kukinga magonjwa mbali mbali. Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali dawa hii ni salama kama itatumiwa kulingana na kipimo sahihi.
Tahadhari ichukuliwe kuhusu matumizi ya dawa hii kwa wanawake wajawazito na kwa watoto chini ya umri wa miaka 12 kwani hakuna taarifa za kutosha kuhusiana na usalama katika makundi haya.
Madhara yanaweza kutokea kwa kutumia dawa lishe hii:
Matumizi ya kipimo kikubwa cha dawa hii ikiwa katika hali yake ya asili (zaidi ya gramu 80) kinaweza kusababisha kizunguzungu,maumivu makali ya kichwa, kushindwa kufumbua macho, kutapika, kuzimia na wakati mwingine inaweza kusababisha kifo. Dawa hii pia inaweza kusababisha mwili kunyong'onyea, kutokuona vizuri, kushtukashtuka kwa misuli na kutetemeka kwa mikono.
-Inasemekana ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi.
Jitahidi kuwa na matumizi ya haya matunda unufaike na uboreshe afya yako.

Endapo unatatizo hili basi wasiliana na Dr. Kamfirimbisi kwa kutumia Simu:+255655531702/+255623450753/+255766105099 au kwa link ya whatsapp hapa chini


Bonyeza Link DR.KAMFIRIMBISI




Contact Form

Name

Email *

Message *