Monday, June 22, 2020

ELIMU YA KIGANJA CHA MKONO


Ni hakika mkono ni sehemu ya jumla ya kuonesha picha ya maisha ya mtu mwenyewe.
Tabia zinazotambuliwa na ilmu hii inategemea tabia ya mtu na mtu mwengine.
Elimu ya kiganja ni njia ya kuelezea mambo yaliopita kwa mtu na yajayo kwa msingi wa maisha ya sasa.
Inahitajika unaposoma kiganja uwe makini zaidi kuangalia michoro ambayo inayoonekana ndani ya kiganja.
Yapo mambo ambayo huepukwa kuyaelezea.
Michoro inaelezea tabia.
Umaarufu.
Safari.
Ubunifu wa kazi.
Kipaji cha muziki.
N.k
Kupitia michoro hiyo utajua mambo muhimu yanayomhusu mhusika wa kiganja hicho.
Usomaji wa kiganja unavutia zaidi.
Umuhimu wa MKONO.
Mkono ni sehemu muhimu ya viungo vya mwanadam .
Hapo mkononi kuna mishipa mingi zaidi kutokea katika UBONGO kuelekea mkononi.
Kuliko eneo lolote la mwili wa binaadam.
Kwa ajili hiyo inaonesha kila kitendo cha akili kitaathiri zaidi eneo la mkono.
MKONO NA UMUHIMU WAKE.
Mkono ni kiungo muhimu ambacho kimejumuisha yafuatayo:-
Vidole.
Kucha.
Kitanga.
Dole gumba.
Eneo la mkono.

KIGANJA KIMEGAWIKA SEHEMU MBILI.
Vidoleni.
Kati kati ya kiganja.
Chini ya kiganja ...karibu ya kiunganikio cha mkono.
Kila eneo hili lina ashiria jambo muhimu katika maisha yako.
VIDOLE.
Jumla ya vidole ni vitano (5) ukijumuisha na kidole gumba.
Na kila kidole kimepewa jina la sayari.
Na kila kidole kinaanisha maana husika ya sayari hiyo.
Japo wapo baadhi ya watu wanavyo vidole sita (6) au vidole saba (7).
Ulaini wa kiganja au ugumu wa kiganja ina ashiria kitu maalumu katika maisha yako.
Kila kidole kina vifundo vitatu ispokua kidole gumba pekee.
Ndio kina vifundo viwili.
Kila kifundo kutokea juu ya ncha ya kidole kinaashiria jambo muhimu katika maisha yako au tabiya zako.
1.Kifundo cha juu cha kucha....kinaashiria utendaji wa fahamu zako.
2.Kifundo cha kati ...kinaashiria vitendo vyako.
3.Kifundo cha chini kabisa....kinaashiria utendaji wa faida uzitakazo.
Au kile ulichokirithi.
Tafauti iliopo ni katika kidole gumba.
Kifundo cha kucha ...kinaashiria utashi wako...au nguvu ulio nazo.
Na kifundo cha mwisho ...kinaashiria fahamu zako au unavyo tafuta hujja (ufahamu).
Haya mambo si rahisi kwa kila mtu kuyaelewa kwa namna inavyozoeleka kwa watu wengi.
Kwa kua kila jambo linazo kanuni zake.
Na pia inahitaji utafiti na umakini wa hali ya juu kuyafahamu mambo haya.
Vidole vyetu na vifundo vyetu tumeumbwa tafauti tafauti...na kiasi inavyokua tafauti ndivyo na maana zake zinavyobadilika.
Hutaliwi kukariri kitu kimoja ...lazima utakosea na kuharibu utaalamu huu.
MKONO AU KIGANJA.
Mkono ni kiungo cha mwili kilichokuepo chini ya vidole vya mkononi na kipo juu ya mkono.
Kunakuepo mistari ndani yake na kunakuepo milima.
Hii misamiati lazima uitambue inaashiria nini inapotajwa?
Milima iliyo maalumu ndani ya kiganja ipo idadi zake ni (8).
IDADI YA MISTARI KATIKA MKONO.
Idadi za mistari mikuu iliopo katika mkono ni saba (7).
Inapatikana mistari midogo ya ziada katika mkono idadi ni kumi (10).
Mistari mikuu inayoonekana zaidi ipo mitatu.
1.Mstari wa Akili.
2.Mstari wa moyo.
3.Mstari wa maisha.
Na kwa mbali sana hupatikana kuonekana mstari wa bahati.
Huu mstari ndio mara nyingi unaoungana na mstari wa akili au mstari wa kichwa kuonesha herufi ya (M). Na hapo imekua baadhi ya watu kujibashiria utajiri au bahati nyingi katika maisha yao.
Bila kujua zinapatikana baadhi ya alama ambazo inakua ni kipingamizi katika hizo bahati...kama yutavyoelekeza na kuzitaja alama hizo.
AINA ZA MIKONO.
Mikono ipo katika maumbile tafauti tafauti.
Na kila umbile la mkono wenyewe inaashiria jambo muhimu kwa mhusika.
Jumla ipo mikono aina saba (7).
VIDOLE .
Vidole ni katika viungo muhimu pia katika sehemu ya mkono.
Kama tulivyoelezea vidole jumla yake ni vitano au baadhi ya watu wanavyo vidole sita au vidole saba.
Na kunakuepo vile vifundo.
Na kila kidole kina maelezo yake ya kukuelezea namna ulivyo wewe.
Na tukumbuke wapo watu wanavyo vidole virefu kuliko watu wengine.
Na wengine wanavyo vidole vifupi kuliko watu wengine.
Na kila mmoja katika wao inaashiria jambo muhimu tafauti na mwenzie.
Aina za vidole ni:
Vidole vifupi.
Vidole virefu.
Vidole laini.
Vidole vyenye vifundo vifundo.
KIDOLE GUMBA.
Wapo watu vidole gumba vyao ni vigumu zaidi.
Wengine vidole vyao vya mzunguuko.
Wengine vya kina kona.
Kwa ujumla vidole gumba vipo tafauti tafauti pia.
KUCHA KATIKA VIDOLE VYA MKONO.
Kucha zipo maumbo tafauti tafauti kwa kila mtu.
Wapo wenye rangi za kucha tafauti pia.
Na kila.kitu hapo kina ashiria jambo muhimu kwa mhusika.
Mkono unao rangi tafauti kwa baadhi ya watu.
Na hili pia lina ashiria jambo muhimu kwa mhusika.
Mpaka hapa inatosha kuwafahamisha kua elimu ya kiganja inasaidia kumjua myu tabiya alio nazo na kuyajua maisha yake vizuri.
Na inasaidia kuwajua watu tabiya zao za kila siku....ambazo wanazificha.
Na kumjua mtu fahamu zake .
Na mengi zaidi ya hayo ambayo yanakuwezesha kujitambua ulivyo kupitia viungo vyako.
JE UNA HERUFI M KATIKA KIGANJA CHAKO? INGIA HAPA UTAZAME HII NDIO MAANA YAKE


Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla.

Pia inasemekana watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara.

Kama una mpenzi mwenye alama 'M' katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu.

Watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao.

Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao.

Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya 'M' basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu.
TAMBUA NAMNA MSTARI KWENYE KIGANJA CHAKO UNAVYOHUSIKA KATIKA MAHUSIANO YAKO NA NDOA YAKO
Mara nyingi watu huenda kwa wanaosoma viganja ili waweze kuelezewa kuhusu wakati wao ujao yaani utabiri na pia bahati zao.Utaalamu huu wa usomaji viganja mara nyingi sana umetumika na huwa kweli kwa asilimia kubwa hasa linapokuja suala la mapenzi na maisha.
Sitakuchosha saaana ila cha kufanya unganisha viganja vyako hapo ulipo.Ile sehemu unakoshikia chakula iwe juu.Mara baada ya kuviunganisha vema hakikisha mistari ya vidole inaendana vema.Baada ya hapo itizame kwa makini mistari mikubwa inayofuatia ilioko chini kabisa baada ya mstari wa mwisho wa kidole kidogo.
Tazama hapa chini kujua matokeo yake:

1)MISTARI INA UREFU SAWA.
Hii inaanisha kuwa mchumba wako atakubaliwa na kupendwa na wengi.Wengi watamfurahia na kumwona mke mzuri na mwema.Pia mtu huyu huwa mkuu,mwenye kujiamini ana asiependa shitukizo.

2) MSTARI WA MKONO WA KULIA UKIWA JUU
Hii inaonesha kuwa inakupasa uwe makini sana na uamuzi wowote ule utako ufanya katika maisha yako.Usikurupuke inapaswa uwe mtulivu sana.
Pia mtu wa aina hii hupendelewa zaidi na wakubwa,pia ana uwezekano wa kuoa au kuolewa na mtu alemzidi umri,mwenye uwezo wa kutambua watu wanaomzunguka,hali iliyopo na asiejali watu wanafikiri nini juu yake.






3) MSTARI WA MKONO WA KUSHOTO UKIWA JUU ZAIDI
Hii inamaanisha kuwa wewe ni mtu jasiri na anaethubutu kukabiliana na changamoto za kimapenzi.Pia hupendelea zaidi vitu visivyo na uhusiano na mahusiano yako.Huyu pia huweza kuoa au kuolewa na mwanafunzi au mgeni wa ng'ambo.Mara nyingi hawa ni watanashati na warembo.



Contact Form

Name

Email *

Message *