Saturday, June 6, 2020

MAJANI YA MWEMBE

TIBA KWA KUTUMIA MUEMBE
Miembe imejaa sana kwenye nchi yetu #Tanzania kila kona ya nchi yetu huwezi kukosa kuona muembe au embe lenyewe . muembe ni tiba ya magonjwa mengi.
Majani ya mwembe:_yanatibu kubana mishipa ya damu (astringent) bi maana yanasaidia sana kufanya damu itembee mwilini kwa wepesi kabisa matumizi unatumia kwa kuyashemsha majani hayo unakunywa glas moja x 2 kwa siku kwa muda wa siku 7
EMBE
Tatizo la kukosa choo, tiba ya fangasi za ndani ,vidonda vya tumbo.
Kula maembe 2 x2 kwa siku ndani ya siku 14 utapata majibu mazuri.
MBEGU_CHANGA_ZA_EMBE
tatizo la kutoa uchafu sehemu za siri. Pia ni tiba ya uke kutanuka (................hapa sisemi ) inawahusu wanawake tuuuu
KUTAPIKA
Chukua majani ya mwembe yaliyosagwa weka mdomoni husitafune wala husimeze sikilizia kama dakika 15 kisha tema bila shaka kwa uwezo wa allah kutapika kutaisha inshaallah
KUTOKA DAMU PUANI
chukua juice ya kokwa CHANGA la embe dondoshea puani vitone vi 3 mala moja tu damu itakata.
TATIZO LA BANDAMA
kunywa juice ya kokwa changa iliyoweka asali mbichi kikombe 1 cha kahawa hasubuh na jion kwa muda wa siku 12 utapona inshaallah
MAUMIVU ZA KIFUA NA KIKOHOZI
Chukua magome ya mti wa muembe yatwange kisha kamua maji yake kunywa kutwa x2 kikombe 1 cha kahawa.
Kwa muda wa siku tano inshaallah utapona.
KUTIBU KISUKARI
chukua majani ya muembe uyaanike juani kisha yasage upate unga wake tumia katika maji ya moto vijiko 2 vya unga uo kwenye maji glas moja kunywa kutwa mala mbili hasubui na jioni kwa muda wa siku 21 utaona matokeo
FAIDA ZA KIAFYA ZA MTI WA MUEMBE/EMBE:
Mti wa mwembe mbali ya kuzaa tunda la embe ambalo hutumika kama chakula au kinywaji ( juisi ) chenye ladha ninayo vutia, una faida lukuki za kiafya kwa mwili wa mwanadamu.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kiafya za mti wa mwembe.
1. MAJANI YA MTI WA MWEMBE :
Majani machanga ya mti wa mwembe yakichemshwa huwa na faida zifuatazo ;
i. Hutibu pumu
ii. Hutibu kifua kikavu
iii. Hutumika katika kuoshea vidonda vitokanavyo na majeraha mbalimbali ( Majani ya maembe yamethibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kukausha majeraha ya vidonda )
iv. Unga wa majani ya mwembe hutumika katika kutunza meno ambapo mtu mwenye matatizo ya meno atatakiwa kusukutua kwa kutumia unga unaotokana na majani ya mwembe.



2. KOKWA LA EMBE
Unga unaotokana na kokwa la embe husaidia kuzuia kuharisha na kuhara damu.
3. TUNDA LA EMBE
i. Ulaji wa tunda la embe husaidia kutibu minyoo na kuzuia uvujaji wa damu ovyo.
ii. Tunda la embe lina vitamin C na hivyo ulaji wake husaidia kuponesha vidonda kwa haraka, hivyo basi mlaji sana wa tunda la embe endapo atapata vidonda basi atapona kwa haraka sana kuliko mtu asiye tumia tunda hili mara kwa mara.
iii. Huwasaidia watu wenye matatizo ya kutokupata choo.
iv. Utumiaji wa maembe mabichi husaidia kuondoa mawe kwenye figo na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji.
v. Embe bichi likichanganywa na chumvi na sukari na kasha kuchemshwa ni tiba ya tatizo la mapigo ya moyo kwenda kwa haraka.
MAGOME YA MWEMBE
Magome ya mti wa mwembe yakichemshwa ni dawa nzuri ya homa.
JUISI YA EMBE :
Juisi ya embe ikichanganywa na maziwa fresh husaidia kurejesha afya ya ,tu aliye dhoofika.
Vile vile kunusa juisi ya embe kunasaidia kuzuia tatizo la kutoka damu puani. Hivyo basi juisi ya embe inaweza kutumika kama huduma ya kwanza kwa mtu anaye tokwa na damu puani.


Endapo unatatizo hili basi wasiliana na Dr. Kamfirimbisi 
kwa Simu:
+255655531702 /+255623450753/ +255766105099 
kutumia Link ya Whatsapp hapo chini akupe ushauri ni bure
Bonyeza Link hii DR.KAMFIRIMBISI ili kuwasiana  




Contact Form

Name

Email *

Message *