Tuesday, May 26, 2020

UGONJWA WA ZINAA



Ugonjwa Wa Kisonono (Gonorrhoea): Chanzo Na Tiba

Ugonjwa wa Kisonono (Gonorrhoea) ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi, wanaume kwa wanawake. Ni ugonjwa unaotibika ingawa kwa miaka ya karibuni, wadudu wa ugonjwa huu wameonyesha kuanza kutosikia tiba zinazotolewa. Kisonono

kisipotibiwa kikamilifu, huweza kuleta madhara ya kudumu kwenye mwili wa mgonjwa na kumfanya aweze kuambukizwa au kuambukiza UKIMWI kwa urahisi. Katika ukurasa huu tutaona chanzo cha ugonjwa huu, dalili zake na mwisho kinga na tiba inayoweza kutolewa kwa ugonjwa huu.
Chanzo Cha Kisonono (Gonorrhoea)
Kisonono ni ugonjwa unaoambukiza kwa ngono – sexually transmitted infection (STI) – na unasababishwa na bakteria
aitwaye Neisseria gonorrhoeae au gonococcus. Bakteria huyu hupenda kuzaliana kwenye maeneo ya joto, yenye unyevunyevu yakiwemo maeneo ya shingo ya uzazi (cervix), nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na mrija wa kutolea mkojo nje (urethra). Bakteria hawa pia huweza kuzaliana kwenye mdomo, mkundu na mara chache kwenye koo na macho.
Kimsingi bakteria hawa hupatikana kwa wingi katika shahawa na usaha unaotoka katika uume wa mwanamme mgonjwa na katika majimaji ya ukeni. Bakteria hawa huambukiza kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa njia zifuatazo:
Ngono zembe kupitia uke, mdomo au mkundu. Mwanamme anaweza kumwambukiza gono mwanamke hata kama hakutoa shahawa (manii) wakati wa kufanya tendo la ndoa
Kuchangia vifaa vya kujistarehesha ambavyo havikuoshwa au kufunikwa na kondomu, kama vibrators na vimwanasesere
vya aina nyingine.
Mama mjamzito mwenye maambukizi anaweza kumwambukiza mtoto anayezaliwa na endapo mtoto huyo hatapewa tiba, anaweza
kupata upofu wa kudumu. Hivyo, mama mjamzito mwenye maambukizi anatakiwa apewe tiba kabla ya kujifungua.
Bakteria wa kisonono hawaambukizi kwa kubusiana, kushikana mikono, kuchangia bafu au taulo, mabwawa ya kuogelea, vyoo, kuchangia vikombe na vyombo ya kulia kwa sababu wadudu hawa wa kisonono hawana uwezo wa kuishi kwa muda mrefu nje ya mwili wa binadamu.
 Dali Za Kisonono
 Sio watu wote wenye kisonono wataona dalili za ugonjwa huu. Pale ambapo mgonjwa ataona dalili, zitaonekana katika siku kama 10 baada ya kupata maambukizi ingawa inaweza ikachukua hadi siku 30. Dalili atakazoziona mwanamme zinaweza kuwa tofauti kidogo na zile atakazoziona mwanamke.
Dalili Za Kisonono Kwa Mwanaume
Kutokwa na uchafu uumeni wenye rangi nyeupe, njano au kijani unaofanana na usaha Maumivu kwenye mapumbu.Maumivu wakati wa haja ndogo Kutokwa na uchafu kwenye mkundu, kuwashwa, kutokwa damu wakati wa haja kubwa.Koo kukauka, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe shingoni. Maumivu kwenye macho, macho kutopenda mwanga mwingi na kutokwa uchafu machoni unafanana na usaha .Maumivu na kuvimba kwenye sehemu za maungio ya mifupa
Dalili Za Kisonono Kwa Mwanamke
Kisonono kinaweza kumsababishia mwanamke kuzaa njiti (mtoto kuzaliwa kabla ya siku) au mimba kuharibika. Mwanamke mwenye kisonono anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa uzazi na kukisababishia kichanga upofu wa kudumu, maambukizi kwenye maungio ya mifupa au maambukizi kwenye damu.
Mwanamme ambaye ana kisonono isiyotibiwa anaweza kupata maumivu makali kwenye mapumbu kutokana na ugonjwa uitwao
epididymo- orchitis na kumsababishia ugumba. Kisonono ambayo haikupewa tiba ya kutosha inaweza kumletea madhara kwenye tezi dume (prostate) na anaweza kupata makovu ndani ya mrija wa kutolea mkojo nje (urethra) na kufanya mkojo utoke kwa shida.
Kisonono huweza kusambaa hadi kwenye mifupa na damu hali ambayo ni hatari kwa maisha. Mtu mwenye gono anaweza kuambukizwa UKIMWI kwa urahisi zaidi.

Tiba Ya Kisonono

Endapo vipimo vimeonyesha kuwa una kisonono, wewe na mwenzi wako wote mnatakiwa kutibiwa kwa kutumia antibiotics na kuacha kujihusisha na masula ya mapenzi hadi hapo tiba itakapokwisha. Baada ya kumaiza tiba, inashauriwa kujipa mapumziko ya angalau miezi 3 kuhakikisha kuwa maabukizi yote yamekwisha.Ndugu msomaji, jisikie huru kuuliza maswali au kutoa maoni uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo, tutafurahi kuona tumekujibu vizuri.
Endapo unatatizo hili basi wasiliana na Dr. Kamfirimbisi kwa Simu:+255655531702 /+255623450753/ +255766105099 
kutumia Link ya Whatsapp hapo chini akupe ushauri ni bure
Bonyeza Link hii DR.KAMFIRIMBISI ili kuwasiana  




Contact Form

Name

Email *

Message *